IMEEELEZWA kuwa Yanga inasubiri neno kutoka kwa Kocha Mkuu, Luc Eymael ili kumalizana na mastaa walio Kwenye rada zao ambao ni Relliants Lusajo na Lukas Kikoti.

Pacha ya Kikoti na Lusajo imekuwa katika ubora msimu huu 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo wamehusika Kwenye mabao 15 kati 34 yaliyofungwa na kosi hilo.

Lusajo ametupia 11 na Kikoti ana mabao manne Kwenye Ligi jambo lililowavutia mabosi wa Yanga na inaelezwa kuwa Simba pia wapo mawindoni kuwawinda nyota hao.

 "Kocha ndiye mwenye maamuzi ambaye anatakiwa kuthibitisha kuwa anahitaji kupata saini zao ama la kisha hesabu za usajili zitaendelea ila sio sasa ni pale muda ukifika," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema:-"Huu sio muda wa usajili mambo bado kabisa hivyo wakati ukifika tutasema nani anaingia na nani anatoka,"

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.