UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa bado una mpango na nyota wao Abdulahman Humud ambaye anatajwa kuwaniwa na Yanga.
Humud ambaye amejiunga na Klabu ya Mtibwa Sugar amekuwa kwenye ubora wake amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga yenye mpango wa kuboresha kikosi chao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa bado hawajafikiria kuuza wachezaji kwa sasa kwa kuwa wana mipango nao.
"Tumekuwa tukskia wachezaji wetu wanawindwa na baadhi ya timu hilo lipo wazi ikiwa ni pamoja na Humud ila hatuna mpango wa kumuuza kwa sasa.
"Bado tuna mipango na wachezaji wetu na hesabu zetu ni kuona kwamba wanakomaa ili waweze kuleta ushindani," amesema
Post a Comment