KOREA Kusini jana Ijumaa iliruhusu ligi yao kuanza kuchezwa ambapo Jeonbuk Hyundai Motors FC iliifunga Suwon Bluewings FC bao 1-0.

Katika mchezo huo wa kwanza, ulishuhudiwa ukichezwa bila ya mashabiki huku kukiwa na baadhi ya sheria mpya zikiwekwa.

Sheria hizo ni; Hakuna kutema mate, chupa za maji za wachezaji zina majina, waandishi wa habari kukaa mita mbili katika chumba cha mikutano, wachezaji na watu wote wa benchi la ufundi kupimwa kwanza afya zao.



Baada ya mchezo huo mmoja wa jana, leo Jumamosi zimechezwa mechi singing tatu ambapo matokeo yake ni; Gwangju FC 0-2 Seongnam, Incheon 0-0 Daegu na Ulsan Hyundai 4-0 Sangju Sangmu.

Wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi walionekana kuvaa barakoa.



Ikumbukwe kuwa, baada ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona, ligi mbalimbali duniani zilisimama na zingine kuahirishwa kabisa.

Hivi karibuni, kumekuwa na matumaini ya ligi kurejea tena ambapo Mei 16, mwaka huu, Bundesliga inatarajiwa kuendelea, kisha La Liga, Premier na Serie A nazo kuna uwezekano zikaendelea Juni, mwaka huu

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.