ANDREY Coutinho, kiungo wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyovikumbuka kwenye ardhi ya Bongo ni pamoja na chakula alichokuwa akikipata wakati akiwa hapa.

Kiungo huyo amesema kuwa kwa sasa anatamani kurudi Bongo na kucheza ndani ya Simba ama Yanga iwapo watahitaji saini yake.

Coutinho alicheza Yanga msimu wa 2014 aliletwa na Kocha Mkuu wa Yanga wa wakati huo ambaye alikuwa ni raia wa Brazil, Maximo akitokea Klabu ya Taubate SP ya Brazil.

Kiungo huyo amesema:-"Ninakumbuka chakula cha Tanzania kwa namna kilivyokuwa cha kipekee hasa ikiwa ni pamoja na ugali ambao nilikuwa ninaupenda sana licha ya kwamba sikujifunza kupika.

"Pia chips mayai ni aina ya chakula ambacho nilikuwa ninapeda kula kwa kweli nimeikumbuka Tanzania na ninaipenda pia," amesema.

Kwa sasa kiungo huyo anakipiga ndani ya Klabu ya Ayutthaya United ya nchini Thailand inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.