UONGOZI wa Azam FC umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, Jumatano ya Machi 4 kuipa sapoti timu hiyo itakapomenyana na Simba ili kuwapa nguvu ya kushinda mbele ya wapinzani hao.
Mchezo huo utakuwa wa pili wa ligi ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere kwa kichwa akimalizia pasi ya Francis Kahata.Utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.
Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa miongoni mwa nguzo muhimu kwa timu ni mashabiki hivyo kujitokeza kwao kwenye mechi kunawapa nguvu ya kupambana
Post a Comment