SADALA Lipangile, nahodha wa KMC amesema kuwa hawakuhitaji kupoteza mchezo wao mbele ya Simba kutokana na nafasi waliyopo kwenye ligi ila walizidiwa mbinu na wapinzani wao.
KMC ilipoteza mchezo wake wa pili mbele ya Simba uliochezwa jana, Machi Mosi Uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 2-0 yote yakifungwa na Luis Miquissone na ule wa kwanza ilichapwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru.
Lipagile amesema: "Tupo kwenye nafasi mbaya kwa sasa hatukupaswa kujilinda ili kuambulia pointi moja, tulifunguka na tulicheza kwa kujiamini makosa yetu ndiyo yametugharimu.
"Tunaweza na tupo vizuri, makosa ambayo tumeyafanya benchi la ufundi lmeona na litayafanyia kazi,".
Lipagile jana, Machi Mosi alipewa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Februari na wadhamini wa ligi ambao ni Voadacom pamoja na king'amuzi cha Azam TV
Post a Comment