BEKI wa kati mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani, ametoa maoni yake kuhusu aina ya usajili ambao mabosi wake wanatakiwa kufanya ili kuhakikisha wanakuwa na kikosi bora kuelekea msimu ujao.

Tayari wapo baadhi ya wachezaji wanaotajwa kutakiwa na Yanga katika kuelekea msimu ujao ambao ni Mussa Mohamed kutoka Nkana FC, Heritier Makambo (Horoya AC), Tuisila Kisinda (AS Vita), Michael Sarpong (Rayon Sports), Yassin Mustapha (Polisi Tanzania), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union) na Abdulhalim Humud (Mtibwa Sugar).

Yondani anasema katika usajili ujao, safu ya ushambuliaji inapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza kwa kuletwa washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kwani hivi sasa wanacheza vizuri, wanatengeneza nafasi nyingi, lakini changamoto inayowakabili ni kushindwa kutumia nafasi hizo kufunga mabao ipasavyo.

Aliongeza kuwa, pia timu yao inahitaji kiungo mwingine mmoja wa pembeni atakayesaidiana na Mghana, Bernard Morrison.

“Timu tuliyokuwa nayo siyo mbaya, lakini tatizo linalotukabili ni safu ya ushambuliaji, tumekosa washambuliaji hatari waliokuwa bora na uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

“Ninaamini kama mabosi wangu wakifanyia kazi hilo kwa kusajili washambuliaji na viungo bora wa kutokea pembeni nina matarajio makubwa ya timu yetu msimu ujao kuwa tishio zaidi.

“Hizo ndiyo sehemu zinazotakiwa kufanyiwa maboresho lakini siyo kusajili wachezaji wengi katika timu watakaokuwa hawana faida yoyote,” alisema Yondani.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga hivi sasa inaongozwa na David Molinga ‘Falcao’, Yikpe Gnamien, Ditram Nchimbi na Tariq Seif.

Yanga ikiwa imefunga mabao 31 katika Ligi Kuu Bara msimu huu, washambuliaji wake wanne wamefunga jumla ya mabao 13. Molinga (8), Yikpe (1), Nchimbi (2) na Tariq (2).

SOURCE: SPOTI XTRA

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.