UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa msimu ujao watabaki ndani ya Ligi Kuu Bara hawatashuka daraja kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Alliance FC inashikilia rekodi ya kuwa timu pekee iliyompiga chini kocha wao aliyeongoza ligi ndani ya dakika 90 ambaye alikuwa ni Athuman Bilal, ’Bilo’ kwenye mchezo wake dhidi ya Mbao FC ambapo iliisha kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Akizungumza na Saleh Jembe,Mwenyekiti wa Bodi mashindano wa Alliance, Yusuph Budodi amesema kuwa wana imani hawatashuka daraja kutokana na mipango mikali waliyonayo.
“Hatukuwa kwenye mwendo mzuri hilo lipo wazi lakini kwa hesabu ambazo tunakuja nazo pale ligi itakaporejea mashabiki wenyewe watatupenda kwani itakuwa ni mwendo wa dozi tu kwa wapinzani wetu, hatushuki daraja,” amesema Budodi.
Alliance FC ipo nafasi ya 18 ikiwa imecheza mechi 29 na kujikusanyia pointi 29 imebakiwa na mechi tisa kukamilisha mzunguko wa pili.
Post a Comment