KUTOKANA na hali ya ukata inayoikabili Ndanda FC, klabu hiyo imeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), liwakopeshe fedha zitakazowasaidia katika uendeshaji ili kumalizia michezo iliyobaki ya Ligi Kuu Bara.
Ndanda ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa michango ya wanachama na wadau, mara kwa mara imekuwa na hali mbaya kiuchumi huku mara kadhaa wakikiri kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji wao.
Katibu Mkuu wa Ndanda, Selemani Kachele, amesema: “Tumesikia kuwa Ligi Kuu Bara inaweza kurejea hivi karibuni kama hali ya mambo itakuwa vizuri, ni jambo la kushukuru lakini sisi kama Ndanda hali yetu ya kiuchumi kwa sasa sio nzuri.
“Kama mnavyojua kuwa klabu hii inaendeshwa kwa michango ya wanachama, hivyo tunaiomba TFF na Bodi ya Ligi kama itafikia uamuzi wa kuirejesha ligi basi watusaidie kutukopesha fedha zitakazotusaidia kuiendesha klabu yetu kumalizia michezo iliyobaki.”
Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Ndanda inashika nafasi ya 16 baada ya kujikusanyia pointi 31 katika michezo yake 29.
SOURCE: SPOTI XTRA
SOURCE: SPOTI XTRA
Post a Comment