ANTONIO Conte, Kocha Mkuu wa Inter Milan inaelezwa kuwa hana mpango wa kumsajili moja kwa moja nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez anayecheza kwa mkopo ndani ya klabu hiyo.
Sanchez amekuwa kwenye kiwango cha chini ndani ya Inter Milan ambapo ameweza kucheza mechi 15 pekee na kufunga bao moja.
Inaelezwa kuwa mabosi wake United hawana hesabu za kumvuta ndani ya klabu hiyo wanataka kumuacha jumlajuma na winga huyo raia wa Chile.
Sanchez amekuwa na hali ngumu ndani ya uwanja tangu alipoondoka Arsenal hata maisha yake ndani ya Inter Milan yalikuwa na maumivu ndani ya uwanja.
Kwa sasa Klabu ya Roma imeanza mikakati ya kuinasa saini ya winga huyo pale atakapotemwa ndani ya Manchester United.
Post a Comment