MOHAMED Hussein, ’Chinga’ straika wa zamani wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kilicho nyuma ya mabao 42 ya mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ni kufuata miiko ya soka kwa umakini
Kagere ni raia wa Rwanda alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Gor Mahia ya Kenya, msimu wake wa kwanza alifunga mabao 23 na msimu huu ligi ikiwa imesimama ameshatupia mabao 19 na kufanya awe na mabao 42.
Akizungumza na Saleh Jembe, Chinga amesema kuwa kinachombeba Kagere kuwa bora na kufunga ni uwezo wake wa kufuata miiko ya soka ambayo wengi huwa inawashinda hasa nidhamu binafsi.
“Wachezaji wengi huwa wanashindwa kueendelea pale walipoishia kwa kushindwa kuwa na nidhamu binafsi nje ya uwanja na ndani ya uwanja ndio maana wanawika mara moja kisha wanapotea tofauti na Kagere anayefuata miiko ya soka.
“Yeye ameweza kujitambua ni nani na anahitaji nini ndio maana msimu uliopita alifunga mabao 23 na sasa anaongoza akiwa na mabao 19 ukitazama alikuwa na nafasi ya kuvunja rekodi yake kwani bado kuna mechi 10 mkononi kwa timu yake, hivyo wengine wanapaswa wajifunze kwake,” amesema Chinga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.