THAMANI YA MZAMBIA ANAYEWINDWA NA SIMBA LAZIMA UKAE
JUSTIN Shonga,mshambuliaji wa kimataia wa Zambia ni miongoni mwa wachezaji ghali sokoni hivyo kibongobongo kuvunja benki ili kuipata saini yake lazima ukae.
Mzambia huyo amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba tangu msimu uliopita wakati ilipokuwa nchini ya Mbelgiji, Patrick Aussems kabla ya kusepa na kwa sasa mikoba yake ipo kwa Sven Vandenbroeck.
Mbelgiji wa sasa wa Simba, Sven amewahi kuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipochipolo’.
Kwa mujibu wa jarida la Kickoff kutoka nchini Afrika Kusini, Mzambia huyo ni miongoni mwa wachezaji kumi wenye thamani kubwa katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini, akiwa na thamani ya euro 600,000 sawa Sh bilioni 1.5 za Kitanzania
Post a Comment