IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa dili lake la kutua Simba aliwashirikisha ndugu zake pamoja na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

Ajibu alikuwa na ofa mbili mkononi msimu wa 2018/19 alipokuwa Yanga ambapo TP Mazembe nao walikuwa wanahitaji saini yake pamoja na Simba.

Yote hayo yalitokana na mchango wake mkubwa ndani ya Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mtengeneza mipango akiwa  na pasi 17 za mabao na alitupia mabao sita.

Ajibu amesema:"Niliwashirikisha ndugu zangu ambao ni familia yangu pamoja na Samatta ambaye aliniambia kuwa hawezi kunichagulia timu zaidi ya kunisharuri nitazame timu itakayonipa furaha."

Kwa sasa Ajibu yupo ndani ya Simba ambapo alisaini kandarasi ya miaka miwili na inaelezwa dau lake lilikuwa ni milioni 80

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.