SIMON Msuva mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga ndani ya Klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morroco amesema kuwa amekumbuka kufunga na kushangilia ndani ya uwanja jambo ambalo kwa sasa haliwezi kutokea.
Kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa ligi nyingi zimesimamishwa kuchukua tahadhari ya maambukizi ikiwa ni pamoja na ile ya Morroco.
Msuva amesema:-"Nimekumbuka kuwa ndani ya uwanja na kushangilia bao ila kwa sasa ni ngumu kuweza kutokea, muhimu kuchukua tahadhari na kuendelea kujilinda."
Post a Comment