MAURICIO Pochettino, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Spurs amesema kuwa bado ndoto yake ya kurejea ndani ya klabu hiyo ipo palepale ili kumalizia kazi aliyoanza.

Spurs ilifanya kazi kwa muda mrefu na kocha huyo ambaye aliifikisha timu hiyo hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/19 ambapo ilipoteza mbele ya Liverpool.

Novemba mwaka jana alipigwa chini ndani ya kikosi hicho kutokana na kikosi hicho kutafanya vizuri ndani ya Ligi Kuu England kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu Jose Mourinho ambaye naye mambo bado hayajawa sawa.

Pochettino amesema:-"Toka nilipoondoka pale ndani ya Spurs ndoto yangu bado haijatimia na kuna mambo ambayo ni lazima nikayamalize na ndoto yangu ni kuwa siku moja nitarudi pale kuendelea pale nilipoishia na ninatakiwa kwenda kumalizia kazi yangu."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.