YAKUB Mohamed, beki wa Azam FC inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kuwaniwa na Simba ambao kwa sasa wanahitaji kuboresha kikosi chao ili kukifanya kiwe bora kimataifa.
Habari zinaeleza kuwa tayari ripoti ya Kocha Mkuu wa Sven Vandenbroeck tayari imeshatua mezani mwa mabosi huku jina la nyota huyo likiwa ni miongoni mwa nyota wanaowindwa.
"Miongoni mwa wachezaji ambao wanahitajika kutua Simba ni pamoja na yule beki rasta wa Azam FC ambaye amekuwa kwenye ubora wake msimu huu hivyo kama mambo yakiwa sawa anaweza kutua Msimbazi.
"Ipo wazi Yakub ana mkataba Azam ila suala la kumpata mchezaji ikiwa anahitajika na timu fulani inawezekana kwa kukaa mezani na kuzungumza, kila kitu kinawezekana," ilieleza.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa bado Yakub ni mali ya Azam hivyo ikiwa Simba ama timu yoyote inahitaji saini yake ifuate utaratibu
Post a Comment