ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amewaambia mabosi wake kuwa anahitaji kusajili majembe matatu ya kazi kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.

Miongoni mwa wachezaji ambao walipitishwa na Cioaba ni pamoja na Obrey Chirwa ambaye ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya mabingwa hao watetezi wa Kombe la Shirikisho.

Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Abdulkarim Amin, 'Popat' amesema kuwa sababu kubwa ya kuwaongezea mkataba nyota ambao wapo ndani ya Azam FC ni kuendeleza mfumo makini huku hesabu ya kuongeza ikiwa ni kati ya wachezaji watatu.

"Tunahitaji kukifanya kikosi kizidi kuwa bora na chenye mwendo uleule bila kupoteza ile falsafa yake na kwenye upande wa kuongeza wachezaji hatutaongeza wachezaji wengi inaweza kuwa kati ya watatu ila hawatazidi saba.

"Yote ni mapendelezo ya kocha ambaye yeye anajua aina ya wachezaji ambao anawahitaji nasi pia tunawapa nafasi ya kuwa ndani ya kikosi bila hiyana."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.