BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anaamini ligi ikirejea atawaonyesha mambo mazuri mashabiki ambayo walikuwa wameyakosa kwa muda mrefu.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama tangu Machi 17 ambapo Serikali iliamua iwe hivyo kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Raia huyo wa Ghana amesema kuwa kwa sasa anafanya mazoezi binafsi nyumbani ili kulinda kipaji chake anaamini mambo yatakuwa vizuri hivi karibuni.
"Mimi ninapenda kucheza mpira na ndiyo kazi iliyonileta hapa Yanga ninaamini ligi ikirejea nitakuwa na nafasi ya kuendelea kuonyesha uwezo wangu wa kile ambacho nilianza kukifanya kwa ajili ya manufaa ya Yanga na furaha kwa mashabiki.
"Kikubwa kwa wakati huu wa mapumziko ya hiyari wachezaji ni muhimu kufanya mazoezi binafsi huku mashabiki na wengine itapendeza iwapo kila mmoja atachukua tahadhari dhidi ya Corona."
Morrison ametupia mabao matatu msimu huu ikiwa ni wa kwanza kukipiga ndani ya Bongo na amecheza mechi 10 za ligi.
Post a Comment