ERASTO Nyoni, beki kiraka ndani ya Simba amewaomba watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Nyoni amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kila mtanzania kuwa balozi kwa mwenzake kwani janga hili linamhusu kila mmoja.
“Ninaamini kwamba kila mmoja anatambua kwamba kwa sasa mambo mengi yamesimama kutokana na uwepo wa janga hili la Corona hivyo ni vizuri ikiwa kila mmoja atachukua tahadhari.
“Mimi nimeanza ambapo nikiwa nyumbani ninawakumbusha wale wanaonizunguka kunawa na kuvaa barakoa ninapenda kuona na watanzania wengine wakazidi kuwa mabalozi ili tuishinde vita hii,” amesema Nyoni. 
Kwenye mabao 63 yaliyofungwa na Simba, Nyoni amefunga bao moja kwa kichwa ilikuwa mbele ya Azam FC Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.