TUISILA Kisinda winga anayekipiga ndani ya Klabu ya AS Vita ya Congo amesema kuwa amefanya mazungumzo na viongozi wa Yanga ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Winga huyo anatajwa kuwa Kwenye mapendekezo ya Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael hivyo mambo yakiwa sawa anaweza kuibuka msimu ujao.

Tuisila amesema:- "Tayari nimefanya mazungumzo na Yanga kuhusu suala la wao kunisajili ili niitumikie timu yao msimu ujao.


 "Bado mazungumzo hayajakamilika kwa sasa na nina amini kwamba mambo yakiwa sawa nitajiunga nayo ili kuitumikia."

Hersi Said Mkurugezi wa Uwekezaji wa GSM aliweka wazi mpango wa kampuni hiyo inayoidhamini Yanga kwenye masuala ya usajili kuwa muda wa usajili ukifika mambo yatakuwa wazi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.