JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa mbali na kufuata program aliyopewa na Kocha Mkuu Luc Eymael anapenda kufanya zoezi la kukimbia ili kuwa bora.
Abdul ni kinara wa kutengeneza nafasi za kufunga mabao ndani ya Yanga ambapo amezitengeneza tano kati ya mabao 31 na zote ametumia mguu wa kulia.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kila siku ni lazima afanye mazoezi ya kukimbia ili kulinda pumzi pale ligi itakaporudi awe bora.
“Kuna program ya mwalimu ambayo tumepewa hiyo ninaifuata na mbali na hiyo pia huwa ninajipa mazoezi ya kukimbia ili kulinda pumzi kwani kukimbia ni moja ya  zoezi ambalo huwa linafanyika pia ndani ya uwanja,” amesema Abdul.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.