WAZIRI wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema kuwa kuna umuhimu wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kufanya mazungumzo na Fifa ili kujua namna gani wanaweza kumaliza ligi kwa wakati.

Mwakyembe amesema kuwa kuna umuhimu wa TFF kukaa pamoja na Fifa ili kuona namna bora itakayowafanya wamalize ligi bila kuwaumiza wachezaji.

"Wakati ule ligi ilipokuwa ikiendelea hali ilipokuwa shwari bila ya uwepo wa Virusi vya Corona kulikuwa na ratiba ngumu kwa timu jambo ambalo tulikuwa tunawashauri TFF kulitazama kwa umakini.

"Unakuta kuna timu ina mchezo Mbeya ikitoka hapo inakwenda Iringa yaani hakukuwa na muda wa timu kupumzika ila kwa sasa kuna umuhimu wa kulitazama hili kwa umakini.

"Rais amesema kuwa anafikiria kuirejesha ligi lakini tutakapoitwa lazima tuwe na mrejesho mzuri wa kuzungumza naye ili apate kutupa ruhusa ya kuendelea na ligi," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.