KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji, amefunguka kuwa kwa sasa hawezi kurejea Dar kwa sababu bado uwanja wa ndege wa nchi yao umeendelea kufungwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Eymael ameweka wazi kwamba bado anaendelea kusalia kwao licha ya kwamba amemisi kurejea Tanzania na kuendelea na mambo yake.

Kocha huyo mwenye uzoefu na soka la Afrika, alirejea kwao Ubelgiji ambapo alienda kukamilisha masuala yake ya ndoa.

Eymael amesema kwamba atarejea Tanzania kuendelea na masuala yake ya ukocha endapo uwanja wao wa ndege ambao unashughulika na safari za kimataifa utakapofunguliwa.

“Nitarudi huko Tanzania pale uwanja wa ndege ukifunguliwa, nashindwa kusafiri kwa sababu hiyo, naendelea kusubiri huku kwetu Ulaya.

“Uwanja wetu wa ndege wa kimataifa bado umefungwa, siwezi kusafiri kwenda kokote pale kwa hiyo nabakia huku hadi vitu vikae sawa, kisha ndiyo nitafanya suala la kurudi,” alisema Eymael

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.