NAHODHA wa PSG, Thiago Emiliano da Silva amesema kuwa wameshinda ubingwa wa maajabu ambao ni mali ya madaktari dunia nzima.

PSG walitangazwa kuwa mabingwa wa Ufaransa, Ligue 1 baada ya ligi hiyo kushindwa kuendelea msimu huu kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Serikali ya Ufaransa imesema kuwa masuala ya michezo yataruhusiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu ambao ni muda wa maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.

Silva amesema kuwa ubingwa huo ni mali ya madaktari wote duniani ambao wanatumia nguvu kubwa kupambana na Virusi vya Corona.

"Huu ubingwa unabaki kuwa alama kubwa kwenye mafanikio yetu, lakini ubingwa huu ni maalum kwa ajili ya madaktari wote duniani ambao wanapambana dhidi ya Corona," amesema beki huyo ambaye pia ni raia wa Brazil.

PSG imetwaa ubingwa ikiwa imecheza mechi 27 ikiwa na pointi 68 ikiwaacha kwa pointi 12 wanaowafuta Marseille ambao wana pointi 56 baada ya kucheza mechi 28. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.