BEKI wa pembeni wa Yanga, Jaffary Mohammed, amesema kuwa anasubiri kusaini mkataba mpya kuendelea kubakia kwenye klabu yake hiyo.
Beki huyo ni kati ya wachezaji wanaomaliza mikataba yao ya kuendelea kukipiga Yanga mwishoni mwa msimu huu, wengine baadhi ni Deus Kaseke, Kelvin Yondani, Juma Abdul na Issa Mohammed ‘Banka’.
Beki huyo anayemudu kucheza nafasi ya kiungo, alijiunga na Yanga kwenye msimu wa 2018/2019 akitokea Majimaji ya mkoani Songea inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka daraja kutoka kwenye Ligi Kuu Bara.
Jaffary amesema kuwa yapo mazungumzo yanayoendelea kati yake na mabosi wake na kama yakienda vizuri, basi haraka atapewa mkataba na kusaini
Post a Comment