THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wanazisubiri Yanga na Simba mezani hali itakapokuwa shwari kuzungumza kuhusu ishu ya kuwahitaji nyota wao wanaokipiga ndani ya mabingwa hao wa Mapinduzi mwaka huu.

Mtibwa Sugar ilitwaa kombe hilo kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Simba kwenye fainali iliyopigwa Visiwani Zanzibar.

Kumekuwa na taarifa kuwa Simba na Yanga zinahitaji kupata saini za wachezaji wao Mtibwa Sugar ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Shomary,Jaffary Kibaya na Abdulhaman Humud.

"Kwa sasa hatujaanza kufikiria kuzungumza na timu ambazo zinahitaji kuwapata wachezaji wetu ikiwa ni pamoja na Job na Kibwana hawa ni wachezaji wazuri ila bado kuna muda ambao tunaweza kukaa mezani kuzungumza kwa sasa acha tupambane na Corona," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.