ADAM Salamba, mshambuliaji wa klabu ya Al-Jahra FC inayoshiriki Ligi Daraja la pili nchini Kuwait amesema kuwa mambo yakibuma kwenye soka ataibukia kuchimba madini.

Salamba ni mshambuliaji wa zamani wa Stand United, Lipuli na Simba ambayo ilimsajili msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Lipuli ambapo alitupia mabao matano ndani ya ligi akiwa Simba.

Salamba amesema:"Kabla ya kuanza kucheza niliwahi kufanya kazi ya kuchimba madini kwenye mgodi wa Acaccia kwa muda wa miezi mitatu hivyo nina uzoefu na uwezo wa kufanya hivyo endapo mambo yatakuwa magumu kwenye soka.

"Nitafanya kazi ya kuchimba madini kwa sababu watu wengi hawajui kwamba kama niliwahi kufanya kazi ya uchimbaji madini kabla sijawa kwenye soka la ushindani."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.