SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa wanajipanga kwa ajili ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara ila hofu yao kubwa ni kuyumba kwa uchumi kutokana na ligi kutarajiwa kuanza kuchezwa bila ya mashabiki.

Aprili 3, Rais wa Tanzania, John Magufuli alisema kuwa anafikiria namna ya kuweza kurejesha ligi ili wachezaji waendelee kufurahia uwanjani na watazamaji kuona kupitia kwenye tv.

Bodi ya Ligi Kuu Bara Tanzania imetoa taarifa kwamba inafikiria kuirejesha ligi mwezi Juni ambapo itachezwa bila ya mashabiki.

Mataso amesema:-"Tunajipanga kurejea uwanjani lakini tunawaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kutuunga mkono kwenye masuala ya fedha,kwa sababu kukosa viingilio vya mashabiki ni tatizo kubwa kwetu." 

Biashara United ipo nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 40.

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.