MARCEL Kaheza, mali ya Simba anayekipiga ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania kwa mkopo amesema kuwa amepata dili la kujiunga na timu ya nchini Ethiopia.
Kaheza amesema kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na miamba hiyo ya soka nchini Ethiopia ambayo ni Klabu ya St.George.
"Kwa sasa mkataba wangu ndani ya Klabu ya Simba unafika tamati mwezi Mei, ninapata ofa nyingi za ndani na nje ya nchi ambazo zinataka huduma yangu na meneja wangu ameniambia kwamba amefikia hatua nzuri ya mazungumzo na Klabu ya St.George.
"Nina ndoto za kuwa mchezaji wa kimataifa hivyo ni suala la muda kuona wapi nitakuwa na nitasaini wapi," amesema.
Kaheza ametupia mabao saba ndani ya Polisi Tanzania na ametengeneza pasi tano za mabao akiwa amehusika moja kwa moja kwenye mabao 12 ya timu yake iliyo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hasmini
Post a Comment