ALLY Niyonzima, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda inaelezwa kuwa ni hatari ndani ya uwanja zaidi ya Bernard Morrison ambaye kwa sasa ndiye nyota namba moja.

Inaelezwa kuwa Yanga ipo kwenye mchakato wa kuisaka saini ya Niyonzima ili kuongeza makali ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Clever Kazungu, Ofisa Habari wa APR ya Rwanda ambao ni washindani wakubwa wa Klabu ya Rayon Sports anayocheza Niyonzima amesema kuwa ni miongoni mwa wachezaji wazuri na hatari ndani ya uwanja.

"Ni miongoni mwa wachezaji ambao wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja na endapo atatua Bongo itakuwa ni habari nyingine kwani ana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi uwanjani huku akiisaidia timu kupata matokeo.

"Ana uwezo wa kukaba, kufunga na kutengeneza mashambulizi pia ana uwezo wa kuchezea mpira vile vitu vinavyofanywa na Morrison kuupanda mpira yeye anaweza pia kufanya hivyo na madoido mengine," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.