DILI la kiungo wa Ufarasa anayekipiga ndani ya Klabu ya PSG, Kylian Mbappe kuibukia Real Madrid limekwama msimu huu mpaka msimu wa 2022.
Inaelezwa kuwa Real Madrid ilikuwa imejipanga kupata saini ya nyota huyo ila kwa sasa imesitisha mpango wake mpaka pale mkataba wake utakapofika ukingoni.
Lengo la Madrid wanahitaji kumpata kiungo huyo bure pale mkataba wake utakapoisha kuliko kupambana kuvunja beki wakati huu thamani yake ikiwa kubwa.
Mbappe amesema anafurahia kuwa ndani ya PSG kwa wakati huu kutokana na sapoti anayopewa kutoka kwa viongozi pamoja na wachezaji wenzake
Post a Comment