HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo ambaye ni raia wa Burundi amesema kuwa mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ana sifa tano ambazo ni muhimu kwa mshambuliaji kuwa nazo.
Kagere alijiunga Simba msimu wa 2018/19 akitokea Gor Mahia ya Kenya, msimu wake wa kwanza alinyanyua makwapa kubeba mataji mawili ambayo ni lile la Ligi Kuu Bara pamoja na ngao ya jamii.
Thiery alisema kuwa mshambuliaji makini ni yule mwenye mwendelezo mzuri na anatimiza majukumu kwa wakati.
“Kagere nimemtazama ni aina ya washambuliaji ambao sio wepesi kukata tamaa mapema, ana spidi akiwa ndani ya uwanja, uwezo wa kukaba , uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi hivi ni vitu vya msingi kwa mshambuliaji kuwa navyo.
“Ninaamini kama ligi ingekuwa inaendelea tungeshudia mengi na kwenye upande wa washambuliaji waliokuwa wanapambana nao yupo na kijana wangu Relliants Lusajo naye ni mpambanaji pia nina amini kuna vitu anajifunza kutoka kwa Kagere,” alisema.
Kagere amefunga mabao 19 na ametoa pasi tano za mabao, msimu wake wa kwanza alifunga mabao 23 na alikuwa ni mfungaji bora.

Chanzo: Championi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.