IKIWA imetupia mabao 31 msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, washambuliaji wanne wa Yanga wametupia mabao 13 wakipotezwa na ile pacha ya Namungo inayowindwa na mabosi wa Yanga.

Kinara wao ni David Molinga ambaye ametupia mabao nane, Yikpe ametupia bao moja, Ditram Nchimbi na Tariq Seif wametupia mabao mawilimawili.

Idadi hiyo ya mabao inapotezwa na ile ya pacha mbili za Namungo ambazo zimetupia mabao 21 ambazo ni Relliants Lusajo na Bigirimana Blaise.


Lusajo ametupia mabao 11 huku Blaise akiwa ametupia mabao 10. Inaelezwa kuwa miongoni mwa waliopendekezwa kuvutwa ndani ya Yanga ni pamoja na hawa wawili ili kuongeza ukali wa safu ya ushambuliaji.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.