PASCAL Wawa beki kisiki wa Klabu ya Simba, raia wa Ivory Coast amesema kuwa kwa sasa anatumia muda mwingi kupiga matizi
makali ili kulinda kipaji chake pale Ligi Kuu Bara itakaporejea.
Miongoni mwa safu ambazo hazijaruhusu mabao mengi kwa msimu wa 2019/20 ni pamoja na ile ya Simba ambayo imefungwa mabao 15 baada ya kucheza mechi 28.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa anaamini kuwa kiwango chake kitakuwa bora iwapo ataendelea kufanya mazoezi bila kuchoka. "Nimekumbuka mpira na shangwe za mashabiki ila sina chaguo kwa sasa ninapambana kujiweka fiti zaidi kwa kufanya mazoezi kila wakati. "Mbali na mazoezi ya ndani ninafanya pia nje ambapo ni kwenye fukwe za Coco Beach huko ninapiga mazoezi na kuchukua tahadhari pia."

Post a Comment