KIUNGO wa Atalanta ya Italia, Andrea Rinaldi, amefariki dunia akiwa na miaka 19 baada ya mishipa yake ya damu katika ubongo kukumbwa na tatizo.
Tatizo hilo lilimpata Ijumaa iliyopita wakati akifanya mazoezi binafsi nyumbani kwake kipindi hiki ambacho kuna katazo la kuepuka mikusanyiko kutokana na uwepo wa corona.
Baada ya kukaa hospitali kwa takribani siku tatu, jana Jumatatu alifariki dunia.
Rinaldi amekulia katika timu ya vijana ya Atalanta na mpaka anafikwa na umauti, alikuwa akiichezea Legnano kwa mkopo ikiwa ni timu inayoshiriki Serie D. Alicheza mechi 23 na kufunga bao moja msimu huu.
Kiungo huyo alikuwa na Atalanta iliyopo Serie A tangu akiwa na miaka 13, ameshinda Kombe la Ligi la vijana chini ya miaka 17 na Super Cup mwaka 2016.
Post a Comment