UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa Simba na Yanga zinapaswa zijipange kunasa saini za nyota wao kutokana na mikataba yao kuwa mirefu kwa wachezaji wao.
Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwindwa na timu hizo mbili za Kariakoo ni pamoja na Dikson Job na Kibwana Shomari ambao wote ni mabeki chipukizi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ni lazima Simba na Yanga zitazame upya sera za kulinda vipaji vya vijana watakaowasajili ili wasipotee katika ramani.
"Timu nyingi zinatazama chuo cha mpira huku makao makuu ili wawasajili lakini wanapaswa wajipange kwani wachezaji wetu wana mikataba mirefu na pia tutaangalia na nafasi zao za kucheza kwani wengi wamekuwa wakiishia benchi kisha wanaachwa kwa sasa lazima tuangalie maslahi yao.
"Ushahidi tunao kwani hata huyu Hassan Dilunga anayetesa kwa sasa aliwahi kusajiliwa na timu hizo akarudi nyumbani ameonekana tena hivyo ameondoka hatutapenda kuona haya yakitokea kwa hawa chipukizi," amesema Kifaru.
Post a Comment