INAELEZWA kuwa Yanga imeongeza juhudi kuinasa saini ya kiungo fundi wa Klabu ya Rayon Sport ya Rwanda Ally Niyonzima kwa ajili ya kumwaga wino ili kuongeza makali ndani ya kikosi hicho msimu ujao.
Habari zinaeleza kuwa tayari Yanga wameshamtumia kopi ya mkataba Niyonzima kwa ajili ya kuupitia kabla ya kusubiri majibu kutoka kwake.
“Kilichofanyika kwa sasa ni kumtumia Niyonzima mkataba wa awali kwa ajili ya kuupitia na kukubaliana juu ya vile ambavyo vimewekwa kwenye mkataba huo.
“Baada ya hapo imetolewa muda kwa ajili ya yeye kurejesha majibu ambapo imefanywa hivyo kwa ajili ya kuepuka kuanza kugombea wachezaji wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa,” kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wa ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alipoulizwa juu ya ishu hiyo hakutaka kuweka wazi zaidi akisema: “Bado dirisha la usajili halijafunguliwa kwa hiyo ni ngumu kuweka bayana ni nani na nani wanasajiliwa, kitu kikubwa tusubiri kuona dirisha likifunguliwa.
Post a Comment