PAUL Nonga nahodha wa Lipuli amesema kuwa kwa siku anapiga mazoezi mara mbili ili kulinda kipaji chake baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Nonga ambaye ni mshambuliaji timu yake ikiwa imetupia mabao 35 amehusika kwenye mabao 15 ambapo amefunga mabao 11 na pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kwa sasa anatumia muda wake mwingi kutimiza program ya mwalimu pamoja na mazoezi yake binafsi.
“Mwalimu ametoa program ambayo ninaifanya asubuhi ili kujiweka fiti zaidi lakini ninaongeza na yangu pia jioni kujiimarisha zaidi.
“Unajua kwa mchezaji ambaye ana malengo ni lazima awe na juhudi binafsi pamoja na kutimiza yale ambayo anaambiwa na benchi la ufundi kwa wakati,” amesema Nonga.
Post a Comment