HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC na mshambuliaji namba moja wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 19, wote raia wa Rwanda mambo kwao bado ni magumu kuhusu kurejea Bongo kwa sasa.
Hitimana na Kagere walikwea pipa kurejea Rwanda baada ya Serikali kusimamisha ligi Machi 17, kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona wanashindwa kurejea nchini baada ya mipaka yao kufungwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa bado nafasi ya kurejea Bongo kwa sasa ni ngumu kwa kuwa mipaka haijafunguliwa.
“Huku Rwanda mambo bado hayajawa shwari sana kwa upande wa mipaka, Serikali haijafungua bado itakuwa ngumu kurejea kwa wakati huu Bongo.
“Lakini jambo pekee la kushukuru Mungu ni kwamba unafuu umeanza kuonekana kidogo kwani kwa sasa tunapata nafasi ya kutoka nje ila kwa tahadhari tofauti na mwanzo,” amesema Hitimana

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.