BARAKA Majogoro, Kiungo wa Polisi Tanzania amesema kuwa msimu ujao ana imani atabaki ndani ya timu yake hiyo kwa kuwa ina nafasi kubwa ya kumpata kutokana na  ushirikiano mkubwa anaoupata kwa sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Majogoro amesema kuwa ishu za kutakiwa na timu kubwa ambazo ni Simba, Yanga na Azam zimefika kwake ila hazijawa rasmi.
“Nimekuwa nikisikia juu ya taarifa za kutakiwa na timu nyingine nje ya Polisi Tanzania ambazo ni Yanga, Simba na Azam, bado haijawa rasmi kwa sasa ninachojua nipo ndani ya Polisi Tanzania na ina nafasi kubwa ya kuwa nami msimu ujao.
“Ninaipa kipaumbele Polisi Tanzania ambapo nipo kwa sasa na mkataba wangu umebakiza miezi michache tu, msimu ukiisha tu na mkataba wangu unaisha pia,” amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.