OBREY Chirwa, mshambuliaji namba moja wa Azam FC anawaongoza washambuliaji wenzake watatu kwenye kuvunja rekodi zao walizoweka msimu uliopita kibabe.
Chirwa msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC 2018/19 akiwa ni ingizo la dirisha dogo alitupia mabao matatu na msimu huu ametupia mabao nane.
Wengine ambao wamevunja rekodi zao kibabe ni pamoja na Paul Nonga anayekipiga Lipuli, msimu uliopita alifunga mabao matano msimu huu ametupia mabao 11 akiwa ndani ya Lipuli.
Yusuph Mhilu akiwa Ndanda alitupia mabao matatu msimu huu akiwa ndani ya Kagera Sugar ametupia mabao 11.
Bigirimana Blaise akiwa Stand United msimu uliopita alitupia mabao 10 msimu huu akiwa Namungo ametupia mabao 10 na kuifikia rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita.
Post a Comment