CLATOUS Chama, kiungo anayekipiga ndani ya Simba msimu huu wa 2019/20 amebadili gia angani kwenye mchango wake wa mabao ya kufunga tofauti na msimu uliopita ambapo alifunga mabao mengi.
Msimu uliopita Chama alifunga mabao saba jambo hilo amelipindua na kuhamishia kwenye kutengeneneza nafasi za mabao ambazo msimu huu ametoa saba na kupachika mabao mawili.
Simba ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 28 na pointi zake 71 kibindoni ina mabao 63 amehusika kwenye jumla ya mabao 9.
Akiwa ametumia dakika 1,745 kwenye mechi 23 ana wastani wa kutengeneza pasi moja ya bao kila baada ya dakika 249.
Ana nafasi ya kupindua tena meza kibabe kwa kufunga mabao matano ili kuvunja rekodi ya mabao saba aliyofunga msimu uliopita kwenye mechi zilizobaki iwapo msimu utaendelea.
Post a Comment