IWAPO mipango itakwenda sawa basi nafasi ya kubaki ndani ya Coastal Union kwa beki wa kati Bakari Mwamnyeto ni ndogo anaweza kuibukia mitaa ya Kariakoo zilipo ngome za Simba na Yanga.

Uongozi wa Coastal Union inaelezwa kuwa wametaja dau la kumuuza nyota huyo ambaye amekuwa kwenye ubora wake na sarakasi zake za usajili wake zilianza tangu msimu uliopita.

Milioni 100 ndiyo ambayo inahitajika ambapo mabosi wa Simba inaelezwa wameanza kujichanga kwani kupitai Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza alisema kuwa hawawezi kushindwa kumpata mchezaji wa ndani iwapo wanamhitaji.

Mwamnyeto amesema kuwa:"Sina mashaka na uwezo wangu popote ninakipiga kwani kazi yangu ni mpira.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.