NYOTA wengi wa kikosi cha kwanza cha Azam FC wapo nje ya nchi kwa sasa jambo linalowapasua kichwa mabosi wao.
Razack Abarola, Yakub Mohamed,Nevere Tigere na Nicolas Wadada wapo nje kwa sasa baada ya kusepa kutokana na mapumziko ya lazima kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.
Kocha Mkuu, Arstica Cioaba na msaidizi wake Vivier Bahati nao hawapo nchini, iwao ligi itaanza hivi karibuni watakuwa kwenye ulimwengu wao katika suala la kutafuta matokeo.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa mipaka ya nyota hao kwa sasa imefungwa hivyo uwezekano wa kurudi Bongo bado ni mdogo.
Post a Comment