ABDULHAMAN Humud, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa miongoni mwa wachezaji wanaocheza kwenye nafasi yake anaowakubali ni pamoja na Papy Tshishimbi na Bernard Morrison wa Yanga.

Pia amemtaja beki kisiki anayekipiga ndani ya Yanga, Kelvin Yondani kuwa miongoni mwa wachezaji makini wawapo uwanjani.

"Wachezaji wengi wanafanya vizuri na kila mmoja ana kitu chake cha kipekee ila kwa harakahara kuna Tshishimbi na Morrison kwa upande wa viungo na beki ni Yondani," amesema.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa kuwindwa na Yanga huku akigoma kuweka bayana ikiwa kuna mazungumzo yameshaanza kwa sasa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.