MICHAEL Sarpong raia wa Ghana, mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda anatajwa kutua ndani ya Klabu ya Yanga.

Nyota huyo amesitishiwa  mkataba wake na Klabu ya Rayon Sports hivyo ni mchezaji huru kwa sasa.

 Msimu uliopita aliweza kuibuka mfungaji bora baada ya kutupia mabao 16.

Sababu ya kupigwa chini ndani ya klabu yake hiyo ni kuskika akizungumza maneno ya kejeli kuhusu rais wa timu yake kwa kuwa hajalipwa mshahara wake. 

Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa sio wakati wa usajili hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.