IMEELEZWA kuwa, Cristiano Ronaldo alikuwa kwenye mpango wa kurudi Manchester United mwaka 2013 baada ya kuondoka hapo mwaka 2009.
Beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amesema kuwa, Kocha Alex Ferguson alikuwa na mpango wa kuwaunganisha Ronaldo na Gareth Bale kikosini hapo kabla ya kustaafu mwaka 2013.
"Alisema kwamba mipango yake kwa asilimia 99 ni kuwa na Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, aliwahitaji ili ashinde tena Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Nilipozungumza na Cristiano, alikubali kurudi na alijiandaa kabisa, lakini wiki mbili mbele, Ferguson akatangaza kustaafu kufundisha,” alisema Evra.
Ronaldo na Bale wamecheza pamoja ndani ya kikosi cha Real Madrid kuanzia 2013 hadi 2018 ambapo Ronaldo amehamia Juventus alipo hivi sasa na Bale amebaki Madrid ingawa hana nafasi kama awali
Post a Comment