MABOSI wa Simba wamesema kuwa wamemruhusu kiungo wao, Ibrahim Ajibu kuondoka muda wowote atakaohitaji na kwenda kujiunga na klabu nyingine itakayomuhitaji kwa masharti, ikiwemo Yanga.

Hii imekuja siku chache tangu taarifa kuzagaa kuwa mchezaji huyo anataka kuondoka kwenye kikosi hicho cha kujiunga na timu moja ya nje ya nchi.

Ajibu alijiunga na Simba msimu huu kwa dau la Sh Mil 80 akitokea Yanga mara baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika. Inaelezwa kuwa timu hiyo imemruhusu kiungo huyo kuondoka lakini lazima masharti maalum yafuatwe.

Mtoa taarifa huyo alisema kiungo huyo wakati anasajiliwa na Simba, viongozi walitegemea kuona makubwa kutoka kwake, lakini imekuwa tofauti baada ya staa huyo kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Wakati anasajiliwa na Simba akitokea Yanga, mabosi walikuwa wana matarajio makubwa ya kumuona Ajibu akicheza kwa mafanikio katika msimu huu, lakini imekuwa tofauti na matarajio yao.

“Hivyo, viongozi wamepata taarifa za Ajibu kutakiwa na moja ya klabu kutoka nje ya nchi, hivyo uongozi umekubali kuachana naye kwani hayupo kwenye mipango ya kocha kuelekea msimu ujao, siyo nje tu ikija timu yoyote hata Yanga tunamruhusu.

“Kikubwa anatakiwa kufuata masharti ya klabu kwa kuiambia timu inayomtaka,”alisema mtoa taarifa huyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.