JAMHURI Kihwelo ‘Julio’, kocha wa zamani wa Simba amesema kuwa mchezaji wa Azam FC, Shabani Idd Chilunda, ni mfano mzuri wa wachezaji wengi wa Kibongo wenye vipaji vya hali ya juu lakini hawajitumi.
Akizungumzia suala la wachezaji wengi wa Kibongo kushindwa kufanya vizuri nje ya nchi, Julio alisema:-“Unajua Tanzania kuna wachezaji wengi wenye vipaji ila hawajitumi, ndiyo maana tunashindwa kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.
“Mfano mzuri ni Chilunda ambaye unaweza kuona kipaji kikubwa alichonacho lakini amekuwa hajitumi kama ambavyo inatakiwa, ndiyo maana anaweza kutamba hapa nchini lakini alishindwa maisha ya nchini Hispania.
“Na hili ndiyo tatizo kubwa la wachezaji wetu, nakumbuka mimi wakati naifundisha Simba tulikuwa tunagombana sana na wachezaji wengi kwa sababu wanataka kusukumwa hadi kwenye suala la mazoezi,” alisema Julio.
Chanzo: Championi
Post a Comment