KIUNGO wa Simba, Luis Miquissone amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ya kupiga mashuti ya mbali katika kipindi hiki cha Corona kwa kuwa anatamani kuona anafunga mabao ya umbali wa mita 20, katika Ligi Kuu Bara.
Luis ambaye amejiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea UD Songo ya Msumbiji alikuwa akicheza kwa mkopo kutokea Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini amesema anaamini atarejea uwanjani akiwa na nguvu.
Luis amesema kuwa moja ya kitu kikubwa anachokifanya kwa sasa ni kuendelea na progamu yake ya kupiga mashuti ya mbali kwa kuwa anataka kuona akifunga mabao ya mita 20 na kuendelea katika michuano ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.
“Naendelea kufanya mazoezi kwa sababu kuna programu ya kocha ambayo nafanya huku nikiwa najilinda na hili janga la Corona ingawa mwenyewe nimejiwekea malengo mengine hasa kwenye upande wa kufunga mabao.
“Sasa hivi najitahidi kuona nakuwa na uwezo wa kupiga mashuti zaidi hasa nje ya eneo la 18 kwa sababu nataka kuona nafanikiwa kwa mabao ya mbali hivyo nimekuwa nikifanya mazoezi kupiga mashuti zaidi,” amesema Luis.
Kiungo huyo mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu katika Ligi Kuu Bara tangu ajiunge na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo.
Post a Comment